Rais Emmanuel Macron, amezungumza kwenye jopo la mwisho katika kilele cha mkutano mjini Paris ambapo baadhi ya viongozi 40, ikiwa ni pamoja na dazeni mbili kutoka Afrika, waziri mkuu wa China na rais wa Brazil walikutana ili kutoa msukumo kwa ajenda mpya ya fedha duniani.
Lengo la mkutano huo ni kuongeza ufadhili wa migogoro katika mataifa ya kipato cha chini na kupunguza mzigo wa madeni yao, kurejesha hali ya kawaida mifumo ya kifedha baada ya vita na kutoa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa kupata maelewano ya hali ya juu ya jinsi ya kukuza idadi ya mipango katika mashirika kama G20, COP, shirika la fedha la kimataifa – IMF, Benki ya Dunia, na Umoja wa Mataifa.
Forum