Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:32

Masomo ya mamilioni ya wanafunzi yaathiriwa na ugaidi Nigeria


Wanafunzi waliyokombolewa kutoka mikononi mwa watekji nyara Nigeria.
Wanafunzi waliyokombolewa kutoka mikononi mwa watekji nyara Nigeria.

Mwaka mpya wa shule nchini Nigeria umeanza mwezi huu wa Septemba lakini zaidi ya shule 600 zimebaki kufungwa kutokana na visa vya utekaji nyara kutoka kwa makundi yenye silaha nchini humo.

Umoja wa Mataifa unasema kwamba Nigeria ina idadi kubwa zaidi ya watoto wasiohudhuria masomo, na kwamba idadi hiyo inaendelea kuongezeka. Kwenye mji mdogo wa Sabo kusini mwa jimbo la Kaduna kundi la wanafunzi limekusanyika pamoja kutokana na ghasia zinazoendelea. Wengi wa wanafunzi hao walifika kwenye kambi maalum za hifadhi wakiandamana na wazazi Novemba mwaka uliopita baada ya kutoroka makwao kutokana na ghasia.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, sayansi pamoja na tamaduni maarufu UNESCO limesema kwamba zaidi ya wanafunzi milioni 20 wa Nigeria hawapo shuleni, likiwa ongezeko la milioni mbili kulinganishwa na utafiti wa Mei mwaka jana. Hata hivyo serikali ya Nigeria imekanusha takwimu hizo ikisema kwamba hali imeimarishwa wakati ufadhili wa sekta ya elimu ukiongezwa.

XS
SM
MD
LG