Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 13:06

Masoko ya hisa yaimarika kufuatia ripoti za chanjo ya Corona


Masoko ya hisa kote duniani yanendelea kunakili faida kubwa kufuatia ripoti kwamba kuna matumaini makubwa ya kupatikana chanjo dhidi ya virusi vya Corona.

Thamani ya hisa katika soko la S&P imepanda kwa asilimia 2.7 baada ya kampuni ya kutengeneza dawa ya Pfizer kusema kwamba chanjo yake ya majaribio dhidi ya virusi vya Corona ni salama kwa asilimia 90.

Kampuni ya Pfizer hata hivyo imesema kwamba chanjo hiyo haitatolewa kwa haraka.

Masoko ya hisa kote duniani yameripoti kwamba thamani ya hisa imeongezeka sana kwa mara ya kwanza katika mda wa miezi miwili.

Masoko ya hisa pia yanaripotiwa kuimarika marudufu kufuatia ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi wa rais wa Marekani.

Bei ya hisa ya kampuni za mafuta imepanda na kuimarisha Imani ya wawekezaji kuhusu ukuaji wa uchumi.

Thamani ya hisa za mafuta katika masoko ya Marekani imepanda kwa asilimia 8.3, kukiwepo matumaini kwamba watu wataanza safari kuelekea sehemu za utalii na safari za ndege kuongezeka kote duniani.

Hisa za maduka ya jumla na nyumba za kukodisha zimepanda kwa kiasi kikubwa, kwa matarajio kwamba watu wengi wataanza shughuli za ununuzi na biashara kwa kasi.

Hisa za kampuni za burudani nazo zimepanda kwa asilimia 34.1.

Mwenyekiti wa kampuni ya kushauri waekezaji ya Bel Air, amesema kwamba masoko ya hisa yameimarika kote duniani kwa sababu watu wana Imani kwamba hatimaye kuna matumaini baada ya mwaka mgumu kiuchumi na janga la kiafya.

Imeyatarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG