Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 17:28

Masoko ya hisa yaanguka, bei ya mafuta yaongezeka


Hisa za masoko ya Asia yalikuwa chini kama zile za Wall Street Alhamisi wakati wasiwasi juu ya uwezekano wa Russia kuivamia Ukraine ukiongezeka(AP Photo/Ahn Young-joon)
Hisa za masoko ya Asia yalikuwa chini kama zile za Wall Street Alhamisi wakati wasiwasi juu ya uwezekano wa Russia kuivamia Ukraine ukiongezeka(AP Photo/Ahn Young-joon)

Masoko ya hisa yameanguka huku bei ya mafuta ikiongezeka kwa zaidi ya dola tano kwa pipa, baada ya Rais wa Russia Vladimir Putin kuanzisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Ukraine.

Mashambulizi hayo yamechochea Washington na Ulaya kuapa kuiwekea Moscow vikwazo vikali, ambavyo huenda vikaathiri uchumi wa dunia.

Masoko ya h isa yameanguka kwa asilimia 4 huku wafanyabiashara wakitathmini namna mataifa ya Magharibi yatajibu uvamizi wa Putin.

Hisa katika soko la Wall Street zimeshuka kwa asilimia 2.5.

Bei ya mafuta ghafi imepanda na kufikia dola 100 kwa pipa mjini London, ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 2014, kutokana na wasiwasi kwamba huenda usafirishaji wa bidhaa hiyo kutoka Russia ukaathirika. Russia ni ya tatu katika uzalishaji wa mafuta duniani.

Nchini Marekani, bei ya mafuta ghafi imepanda na kufikia dola 98 kwa pipa. Bei ya ngano na mahindi vile vile imepaanda.

Mjini Brussels, rais wa tume ya umoja wa ulaya Ursula Von der Leyen amesema kwamba mataifa 27 ya umoja huo yamepanga kutangaza vikwazo vikali dhidi ya Russia, na kwamba rais atawajibishwa ipasavyo.

XS
SM
MD
LG