Upatikanaji viungo

Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 21:20

Imran Khan awasili Russia kwa mazungumzo na Vladmir Putin


Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan akizungumza katika mahojiano na Reuters mjini Islamabad

Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan aliwasili Russia Jumatano kwa mkutano muhimu na Rais Vladmir Putin.

Maafisa wanasema viongozi hao wawili watatathmini uhusiano wa nchi hizo mbili pamoja na ushirikiano wa nishati. Televisheni ya Pakistan PTV inayomilikiwa na serikali ilitangaza moja kwa moja kuwasili kwa Khan katika uwanja wa ndege wa Moscow ambapo Khan alipokelewa na naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia, Igor Morgulov.

Khan ndie kiongozi wa kwanza wa kigeni kuzuru Moscow tangu Putin kutambua uhuru wa Jamhuri zilizojitenga na Ukraine za Donetsk na Luhansk mapema wiki hii na kupeleka wanajeshi huko. Hatua hiyo ya Russia ilizidisha mvutano na nchi za magharibi na kuibua vikwazo vipya vya kimataifa dhidi ya Russia.

Viongozi hao wawili wanapanga kujadili masuala makuu ya ushirikiano baina ya nchi mbili hizo, pamoja na masuala ya kikanda ikihusisha maendeleo ya Asia kusini, Peskov alisema. Safari hiyo ni ya kwanza kwa Waziri Mkuu wa Pakistan kwenda Russia tangu mwaka 1999.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG