Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 21:25

Maafisa wa chama cha Demokratik wamfungulia mashtaka Donald Trump


Republican presidential candidate Donald Trump speaks at a rally Sunday, Oct. 30, 2016, in Las Vegas.
Republican presidential candidate Donald Trump speaks at a rally Sunday, Oct. 30, 2016, in Las Vegas.

Maafisa wa chama cha Demokratik hapa Marekani wamemfungulia mashtaka mgombea kiti cha rais wa chama cha republican Donald Trump katika majimbo manne yenye ushindani mkali Jumatatu, kwa lengo la kuzuia juhudi za kuweka waangalizi wake kwenye vituo vya kupiga kura.

Maafisa wa chama cha Demokratik wanasema mpango huo una lengo la kuwabugudhi na kusababisha kitisho kwa wapiga kura na jamii ya wachache hapo Novemba 8 siku ya uchaguzi.

Mashtaka yamefikishwa mbele ya mahakama ya serikali kuu katika majimbo ya Pennsylvania, Nevada, Arizona na Ohio. Na maafisa wa chama cha Demokratik wanatoa hoja kwamba maafisa wa chama cha Republican wameanzisha kampeni ya uwanaharakati kuwatishia wapigaji kura jambo ambalo linakiuka kanuni ya haki za upigaji kura ya 1965 na sheria ya 1871 iliyolenga kundi la ubaguzi la Ku Klux Klan.

Kampeni ya Trump haijatoa taarifa yeyote kuhusiana na mashtaka hayo tangu mwezi Agosti Trump amewahimiza wafuasi wake kusimamia vituo vya kupiga kura siku ya uchaguzi ili kuangalia kama kuna ishara za ubadhirifu wa uchaguzi wa aina yeyote.

XS
SM
MD
LG