Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 06, 2023 Local time: 07:48

Mashirika ya Umoja wa mataifa yaeleza Tigray yakumbwa na njaa


Eneo la Tigray nchini Ethiopia.
Eneo la Tigray nchini Ethiopia.

Uchambuzi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na vikundi vya misaada unakadiria kuwa karibu watu 350,000 katika mkoa wa Tigray uliokumbwa na mizozo nchini Ethiopia wako katika hali ya njaa, kulingana na hati ya ndani ya Umoja wa Mataifa ambayo Reuters waliipata Jumatano.

Serikali ya Ethiopia inapingana na uchambuzi wa Uainishaji wa Awamu ya Usalama wa Chakula (IPC), kulingana na maelezo ya mkutano juu ya hali ya Tigray ya Kamati iiitwayo Inter-Agency Standing Committee (IASC) iliyoundwa na wakuu wa nchi zisizopungua 18 za Umoja wa mataifa na mashirika wasio Umoja wa mataifa mashirika.

Juu ya hatari ya njaa, ilibainika kuwa takwimu za uchambuzi wa IPC ambazo hazijachapishwa zilikuwa zikipingwa na serikali ya Ethiopia, haswa watu wanaokadiriwa kuwa 350,000 kote Tigray wanaaminika kuwa katika hali ya njaa katika hatua ya IPC 5, ilisema hati ya Juni 7.

XS
SM
MD
LG