Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:16

Misaada yafika mji uliokuwa hauingiliki Syria


Mashirika ya kutoa misaada kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minne yameweza kupeleka misaada kwa mji wa Syria uliozingiwa kufuatia idhini ya serikali ya kuruhusu misaada kwenye maeneo yalioshikiliwa na waasi.

Usiku wa kuamkia leo, shirika la Syrian Arab Red Crescent pamoja na Umoja wa Mataifa wameweza kupeleka misaada ya kudumu mwezi mmoja pamoja na madawa kwa watu wa Daraya eneo lililo kusini magharibi mwa mji mkuu wa Damascus ambalo lililkuwa limeshikiliwa na waasi tangu 2012.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Jans Laerke, amesema kuwa wamepeleka chakula cha kutosha kuwalisha watu 2,400 kwa kipindi cha mwezi mmoja pamoja na madawa ya kutosha idadi ya watu inayokisiwa kuwa 4,000.

XS
SM
MD
LG