Mashambulizi hayo, ambayo mtu mwenye umri wa miaka 29 aliuawa pia katika mkoa wa kaskazini mashariki wa Kharkiv kulingana na maafisa, ni ya hivi karibuni katika mfululizo wa mashambulizi ya usiku yaliyofanywa na Russia, wakati Kyiv ikiweka nguvu zake kwenye mashambulizi ya kujibu.
Jeshi la anga la Ukraine limesema makombora manane ya kutoka ardhini na ndege zisizo na rubani 35 zilitumiwa katika mashambulizi hayo. Vituo vya ulinzi wa anga vilifanikiwa kuangusha ndege 20 zisizo na rubani na makombora mawili ya baharini, jeshi hilo limesema.
“Kutokana na mapigano hayo ya angani, mabaki kutoka kwa moja ya ndege zisizo na rubani yalianguka kwenye ghorofa ya juu ya jengo la makazi ya raia na kusababisha moto,” msemaji wa jeshi eneo la kusini Natalia Humeniuk amesema kuhusu shambulio hilo kwenye mji wa Odesa.
Maafisa wa Ukraine wamesema watu watatu waliuawa wakiwemo wanandoa waliokuwa wanaishi kwenye ghorofa ya nane ya jengo hilo na mwanaume aliyekuwa nje wakati wa shambulio hilo.
Forum