Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 02:26

Mashambulizi ya maafa makubwa Syria


Zaidi ya watu 55 wauawa 370 wajeruhiwa

Mamlaka za Syria zinasema mashambulizi mawili ya mabomu yaliyofanywa na wahanga wa kujitolea Alhamis mjini Damascus yameuawa watu 55 na kujeruhi wengine 370, hili likiwa shambulizi lenye maafa makubwa zaidi kufanyika nchini humo tangu upinzani kuanza maandamano dhidi ya serikali yapata miezi 14 iliyopita. Milipuko hiyo pacha ilifuatana katika muda wa dakika moja na kutingisha mji mkuu wa Syria wakati wa harakati za asubuhi watu wakielekea kwenye shughuli zao. Mashambulizi hayo yaliteketeza magari dazeni kadha na kusababisha wingu jeusi la moshi. Yalitokea katikati ya barabara karibu na majengo mawili ya ulinzi mali ya serikali. Televisheni rasmi ya Syria ilisema washambuliaji hao walitumia magari mawili kutekeleza mashambulizi hayo asubuhi na mapema Alhamis katika eneo la Qazaz mjini Damascus.

XS
SM
MD
LG