Zaidi ya watu 4,000 wamekimbia kutoka maeneo yanayozunguka mkoa wa kaskazini mashariki mwa Ukraine wa Kharkiv tangu Ijumaa, wakati Russia ilipoanzisha mashambulizi ya kushtukiza, gavana wa eneo hilo alisema Jumapili.
Kwa jumla, watu 4,073 wameondolewa, Oleg Syniehubov aliandika kwenye mitandao yake ya kijamii. Syniehubov amesema mwanamme mwenye miaka 63 aliuawa kwa kupigwa risasi katika kijiji cha Glyboke na pia mtu mwingine mwenye miaka 38 alijeruhiwa katika mji wa mpakani wa Vovchansk wenye wakaazi wapatao 3,000 kabla ya shambulizi la Ijumaa la Russia.
Wakitumia risasi na makombora, vikosi vya Russia vimekuwa vikishambulia miji na vijiji katika eneo hilo. Angalau kitengo kimoja cha Ukraine kimejiondoa kutoka mkoa wa Kharkiv wakati vikosi vya Russia vinachukua udhibiti katika kile kinachoitwa “maeneo ya amani” kwenye mpaka wa Russia.
Forum