Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 22:45

Mashambulizi ya jeshi la Marekani na Uingereza yaua watu 11 nchini Yemen


Picha hii inaonyesha ndege ya Kijeshi ya Marekani ikiwa kwenye meli ya kivita katika Bahari ya Sham, ikishambulia ngome za Wahouthis, Februari 24, 2024.
Picha hii inaonyesha ndege ya Kijeshi ya Marekani ikiwa kwenye meli ya kivita katika Bahari ya Sham, ikishambulia ngome za Wahouthis, Februari 24, 2024.

Mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na muungano wa jeshi la Marekani na Uingereza yalilenga miji ya bandari na miji midogo magharibi mwa Yemen Jumatatu, na kuua watu 11 na kujeruhi wengine 14, msemaji wa serikali ya Yemen inayotambuliwa kimataifa ameliambia shirika la habari la Reuters.

Mashambulizi 17 ya anga yaliripotiwa nchini humo, ikiwemo katika mji mkuu wa bandari wa Hodeidah na bandari ya Ras Issa, kulingana na kituo cha televisheni cha Wahouthi, Al Masirah.

Mashambulizi hayo yamefanyika siku chache baada ya vifo vya kwanza vya raia na upotezaji wa meli tangu waasi wa kiHouthi wanaoungwa mkono na Iran kuanza kushambulia meli za biashara mwezi Novemba wakidai kushikamana na Wapalestina wanaoshambuliwa na Israel.

Mashambulizi hayo yamefanyika sambamba na siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Licha ya mashambulizi ya kulipiza kisasi ya muungano wa Marekani na Uingereza na majeshi mengine ya majini, Wahouthis walizidisha mashambulizi yao dhidi ya meli za biashara katika moja ya njia yenye shughuli nyingi za usafiri wa meli za biashara duniani.

Wahouthis siku ya Jumatano waliua wafanyakazi watatu wa meli ya Ugiriki ya True Confidence iliyokuwa na bendera ya Barbados, katika shambulio nje ya bandari ya Eden.

Forum

XS
SM
MD
LG