Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 21:53

Mashambulizi ya jeshi la Israel yaua Wapalestina 17 Ukanda wa Gaza


Moshi na moto watanda kutoka jengo lililoharibiwa na shambulizi la Israel katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat, katika Ukanda wa Gaza, Novemba 28, 2024. Picha ya Reuters
Moshi na moto watanda kutoka jengo lililoharibiwa na shambulizi la Israel katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat, katika Ukanda wa Gaza, Novemba 28, 2024. Picha ya Reuters

Mashambulizi ya kijeshi ya Israeli yameua Wapalestina 17 katika Ukanda wa Gaza leo Alhamisi, madaktari wamesema, huku vikosi vikizidisha mashambulizi yao katika maeneo ya kati na vifaru kuingia zaidi kaskazini na kusini mwa eneo hilo.

Mashambulizi hayo yamejiri siku moja baada ya Israel na kundi la Hezbolla, linaloungwa mkono na Iran kuanza usitishwaji wa mapigano nchini Lebanon, na kumaliza zaidi ya mwaka mmoja wa uhasama na kuongeza matumaini miongoni mwa Wapalestina huko Gaza, kwa makubaliano sawa na Hamas, kundi linalotawala eneo hilo.

Watu sita waliuawa katika mashambulizi mawili tofauti ya anga, yaliyolenga nyumba moja na eneo lililo karibu na hospitali ya Kamal Adwan, huko Beit Lahiya, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, wakati wengine wanne wakiuawa kufuatia shambulio la Israel liligonga pikipiki huko Khan Younis kusini.Huko Nuseirat, moja ya kambi nane za kihistoria za wakimbizi za Gaza, Ndege za Israel zilifanya mashambulizi kadhaa na watu wasiopungua saba waliuawa katika mashambulizi hayo, maafisa wa afya walisema.

Forum

XS
SM
MD
LG