Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 10, 2025 Local time: 22:54

Mashambulizi ya Israel yazidi kuleta maafa Gaza


Israel iliwashambulia wanamgambo wa Hamas katika miji mikubwa huko Ukanda wa Gaza, Alhamisi, na kusababisha vifo vya watu 350 na maelfu ya raia wa Palestina wakitafuta makazi kukimbia athari za vita.

Watu wengi wa Gaza, waliokimbia makazi yao walijazana Rafah, katika mpaka wa kusini pamoja na Misri, ambapo vipeperushi vya Israel viliwataka Wapalestina kukimbia ili wawe salama.

Lakini wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas, imeripoti vifo vya takriban watu 37 katika mashambulizi ya anga ya usiku yaliyofanywa na Israeli.

Jeshi la Israel, Alhamisi liliwashutumu wanamgambo wa Hamas kwa kufyatua roketi kutoka maeneo ya karibu na Rafah karibu na eneo la juhudi za kibinadamu.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema hakuna maeneo yaliyo salama Gaza. Zaidi ya asilimia 85 ya idadi ya watu zaidi ya milioni 2 katika eneo hilo tayari wamekimbia makazi yao.

Forum

XS
SM
MD
LG