Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 04:43

Mashambulizi ya angani yaliyo fanywa na jeshi la Israeli yaua Wapalestina wasiopungua 17


Mazishi ya Wapalestina waliouawa katika mashambulizi yaliyofanywa na Jeshi la Israeli huko Rafah, in Khan Younis.
Mazishi ya Wapalestina waliouawa katika mashambulizi yaliyofanywa na Jeshi la Israeli huko Rafah, in Khan Younis.

Mashambulizi ya anga ya Israeli Jumanne yameuwa Wapalestina wasiopungua 17 katika kambi mbili za wakimbizi za kihistoria huko  Ukanda wa Gaza na vifaru vya Israeli viliingia ndani zaidi katika mji wa kusini wa Rafah, wakazi na wafanyakazi afya walisema.

Wakazi wameripoti mashambulizi ya mazito ya mabomu yanayofanywa na vifaru na ndege katika maeneo kadhaa ya Rafah, ambapo zaidi ya watu milioni moja wametafuta hifadhi huko kabla ya mwezi Mei. Wengi kati ya watu hao wamekimbilia upande wa kaskazini tangu wakati huo wakati majeshi ya Israeli yalipouvamia mji huo.

“Rafah inashambuliwa kwa mabomu bila ya uingiliaji kati wowote wa kimataifa, mkaliaji kimabavu ( Israel) yuko huru kufanya chochote hapa,” mkazi wa Rafah na baba wa watoto sita aliiambia Reuters kupitia program ya app ya Chat.

Vifaru vya Israeli vimekuwa vikifanya operesheni yake ndani ya maeneo ya Tel Al-Sultan, Al-Izba, na Zurub upande wa magharibi mwa Rafah, na pia Shaboura katikati ya mji huo.

Kifaru cha Jeshi la Israeli kikifanya operesheni yake Mei 30, 2024 eneo linaloizunguka Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.
Kifaru cha Jeshi la Israeli kikifanya operesheni yake Mei 30, 2024 eneo linaloizunguka Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Pia wameendelea kukalia kimabavu maeneo jirani upande wa mashariki na nje ya mji na pia kwenye mpaka wa Misri na kivuko muhimu cha mpakani huko Rafah.

“Kuna majeshi ya Israeli katika maeneo mengi zaidi, kuna mapigano makali ya kujihami, yanawafanya walipe thamani kubwa lakini uvamizi siyo katika maadili na wanauharibu mji na kambi za wakimbizi,” mkazi huyoi alisema.

Maafisa wa afya wa Palestina walisema mtu mmoja aliuawa asubuhi na shambulizi la Israel upande wa mashariki mwa Rafah. Wafanyakazi wa afya walisema wanaamini wengine wengi wameuawa katika siku zilizopita na wiki kadhaa lakini timu za uokoaji hazikuweza kuwafikia.

Jeshi la Israeli lilisema lilikuwa linaendelea na “operesheni inayoongozwa na taarifa za kijasusi, kwa umakini” huko Rafah, wakiwauwa Wapalestina wengi wenye bunduki katika kipindi cha siku moja iliyopita katika mapambano ya karibu na kukamata silaha kadhaa. Jeshi la anga lilishambulia darzeni ya malengo katika eneo la Ukanda wa Gaza siku moja iliyopita, iliongeza.

Katikati mwa Ukanda wa Gaza, mashambulizi mawili tofauti ya anga yalipiga nyumba mbili na kuua Wapalestina 17 huko Al-Nuseirat na Al-Bureiji, maeneo mawili yaliyotengwa kwa ajili ya kambi za wakimbizi ambayo ni makazi ya familia kadhaa na vizazi vya watu ambao walikimbilia Gaza katika vita vya mwaka 1948 wakati taifa la Israel lilipoundwa, wafanyakazi wa afya walisema.

Forum

XS
SM
MD
LG