Kwanza yaliharibu madirisha, na sehemu kubwa ya paa la chuo kikuu cha taifa cha Agrarian kilichopo nje kidogo ya mji wa Lviv, ambapo Stepan Bandera, shujaa wa Ukraine ambaye Kremlin inamchukulia kama mnyama alisoma.
Mashambulizi hayo yamefanyika katika kipindi ambacho ni maadhimisho ya miaka 115 ya kuzaliwa kwa Bandera.
Shambulizi la pili liliharibu makumbusho ambayo yametengwa kwa ajili ya Roman Shukhevych.
Wote wawili hao ni vielelezo muhimu kwa kudai utaifa wao kutoka kwa utawala wa Kisovieti, ambao ulikuwa ukihusishwa na kundi la wanamgambo wa Ukraine, UPA ambao ulipambana na vikosi vya Kisovoeti, katika vita vya pili vya dunia.
Forum