Ufalme huo umeongeza udhibiti katika eneo la mpakani na Syria katika miaka ya hivi karibuni na majeshi yake kwa kipindi fulani hutangaza operesheni mbalimbali kuzuia dawa za kulevya na majaribio ya ulanguzi wa silaha kutoka maeneo jirani na nchi hiyo iliyoharibiwa na vita.
“Ndege za kivita za Jordan zilitekeleza mashambulizi ya anga yakilenga maeneo ya makazi na ghala huko kusini mashariki ya mkoa wa Sweida, yaliouwa watu wasiopungua tisa, wakiwemo wasichana wawili na wanawake wanne,” kituo cha uangalizi cha haki za binadamu cha Syria (Syrian Observatory for Human Rights) kilisema, kikieleza kuwa ni “mauaji.”
Shambulizi la kwanza katika nyumba iliyoko kijiji cha Urman liliuwa mwanaume mmoja, mkewe na mabinti zake wawili, pamoja na kaka yake na mkewe, kilisema kikundi hicho cha ufuatiliaji chenye makao yake Uingereza.
Miili ya mwanaume, mama yake na shangazi yake ilikutwa katika nyumba ya pili iliyokuwa imelengwa, iliongeza kusema kituo hicho cha ufuatiliaji, ambacho kinategemea vyanzo vya mitandao mbalimbali viliyoko Syria kwa ajili ya ripoti zake.
Tovuti ya habari ya Suwayda24 iliripoti kuwa, inawezekana mashambulizi ya angani “ yalifanywa na jeshi la anga la Jordan” na kuua watu wasiopungua 10 huko Urman.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.
Forum