Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 14:39

Shambulizi nchini Mali laua walinda amani


Watu wanne wameuwawa katika mashambulizi mawili tofauti kwenye kambi za Umoja wa Mataifa huko Mali tangu Jumanne.

Mlinda amani mmoja aliuwawa katika shambulizi la roketi Jumanne usiku na kusababisha watu 10 wengine kujeruhiwa katika kambi ya Umoja wa Mataifa ya huko Gao ijulikanayo kama MINUSMA.

Shambulizi la pili lilitokea Jumatano asubuhi katika operesheni ya kuzuia uchimbaji (UNMAS) katika mtaa mwengine wa Gao na kusababisha vifo vya watu watatu.

Siku ya Jumapili watumishi watano wa ofisi ya kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa huko Mali waliuliwa na mmoja kujeruhiwa katika shambulizi la kushtukiza.

XS
SM
MD
LG