Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 10, 2025 Local time: 03:53

Mashambulizi makali ya jeshi la Israel yanaendelea Rafah


Nyumba iliyoharibiwa kutokana na mashambulizi ya mabomu katika ukanda wa Gaza, May 22, 2024
Nyumba iliyoharibiwa kutokana na mashambulizi ya mabomu katika ukanda wa Gaza, May 22, 2024

Vifaru vya Israel vimesonga mbele na kuingia katika wilaya yenye idadi kubwa ya watu ndani ya Rafah leo Jumatano, huku mabomu kadhaa yakiangushwa kusini mwa mji wa Gaza katika operesheni ambayo imetajwa kuwa nzito sana tangu Israel ilipoanza mashambulizi katika sehemu hiyo mwezi huu.

Mashambulizi ya Israel katika sehemu ya kusini mwa Rafah yamepelekea maelfu ya watu kuondoka sehemu hiyo ambayo imekuwa ikikaliwa na watu milioni 2.3 waliokimbia vita.

Njia kuu zilizokuwa zikitumika kusafirisha misaada kuingia Gaza zimefungwa, hatua ambayo imepelekea wasiwasi wa kutokea vifo vya watu kadhaa na njaa.

Israel imesema kwamba haina jingine la kufanya kando na kuushambulia mji huo ili kuwamaliza wanamgambo wa Hamas wanaoaminika kujificha Rafah.

Wakaazi wa Rafah wamesema kwamba ndege zisizokuwa na rubani za Israel zimeshambulia kitongozi cha Yibna usiku wa kuamkia leo na kupiga boti za uvuvi, baadhi zimewaka moto kwenye ufuo wa Rafah. Jeshi la Isral halijatoa taarifa kuhusu operesheni yake ndani ya Rafah.

Forum

XS
SM
MD
LG