Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:44

Mashambulizi dhidi ya raia na maafisa wa usalama yameongezeka Niger


Wapiganaji wa kundi la waasi wa ki-Taureg wa Niger MNJ wakiendesha magari yenye silaha kaskazini mwa Niger.
Wapiganaji wa kundi la waasi wa ki-Taureg wa Niger MNJ wakiendesha magari yenye silaha kaskazini mwa Niger.

Ongezeko la mashambulizi ya makundi wa wapiganaji magharibi mwa Niger tangu mwezi Januari, limelazimisha watu kadhaa kutoroka nyumbani kwao na kutafuta mahali salama.

Kulingana na shirika la umoja wa mataifa la kushughulikia wakimbizi, idadi ya watu wanaoondoka makwao kwa lazima imeongezeka katika mda wa miezi 5 iliyopita kutokana na ongezeko la mashambulizi ya makundi ya wapiganaji wanaoshambulia raia na maafisa wa usalama.

Shirika hilo la umoja wa mataifa limehesabu visa 136 kati ya mwezi Januari na April mwaka huu.

Raia 43 waliuawa na 22 kutekwa nyara katika kipindi hicho katika sehemu za Torodi, Tera na Gotheye eneo la Tillaberi, mpakani na Burkina Faso na Mali.

Zaidi ya watu 34,000 wametoroka makwao kutokana na mashambulizi hayo.

XS
SM
MD
LG