Mamlaka za usalama Ubelgiji zinaendelea kumtafuta mmoja wa watu wanaoaminika kuhusika na mashambulizi ya Jumanne ya uwanja wa ndege na kituo cha treni mjini Brussels, Ubelgiji ambayo yaliuwa watu 31 na kujeruhi wengine 271.
Mwendesha mashitaka wa serikali, Frederic Van Leeuw, alithibitisha ndugu wawili Khalid na Brahim el-Bakraoui walikuwa walipuaji wa kujitoa muhanga katika mashambulizi hayo.
Khalid alijilipua yeye mwenyewe katika kituo cha treni cha Maelbeek na ndugu yake Brahim alijilipua kwenye uwanja wa ndege, kwa mujibu wa Van Leeuw.
Mamlaka za usalama bado hazijathibitisha kuwatambua wanauwe wengine wawili walioonekana katika picha za video zilizochukuliwa na kamera za usalama za CCTV katika uwanja wa ndege.
Van Leew amesema maafisa wa usalama wamekamata milipuko, vifaa vya milipuko na bendera ya Islami State ilikiwa miongoni mwa na vifaa vingi vya milipuko katika mtaa wa Schaerbeek, katika mji mkuu Brussels.