Stern alipatwa na kiharusi Disemba 12 na kufanyiwa matibabu ya upasuaji wa dharura.
Stern ambaye aliongoza NBA kwa miaka 30 alipatwa na kiharusi Disemba 12 na kufanyiwa matibabu ya upasuaji wa dharura.
Stern ataenziwa kama kiongozi aliyeinua umaarufu wa ligi hiyo baada ya kuchukua uongozi wake mwaka 1984.
Chini ya uongozi wake NBA iliongeza timu saba mpya, kuunda ligi ya wanawake WNBA na ligi ndogo zinazojulikana kama G league kuandaa wachezaji kuingia katika ligi kubwa.
David stern pia alihusika katika kufanya NBA kuwa ligi ya kimataifa kwa kusajili wachezaji kadha kutoka nje ya Marekani na kufanya mechi za NBA kutangazwa katika zipatazo 200 duniani. Stern alisimamia ukuaji wa Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani hadi kufikia kuwa ni mshikamano wa kimataifa,
Wachezaji mbalimbali ambao ni nyota wa mchezo wa mpira wa kikapu akiwemo mchezaji mashuhuri Michael Jordan wamemwagia sifa kemkem Stern kwa kunyanyua mchezo wa mpira wa vikapu kufikia hadhi ya kimataifa, jambo lililopelekea kuwasaidia wao kupata umashuhuri katika maisha yao ya mpira wa vikapu.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.