Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 23:01

Maseneta wanne Marekani wamtaka Trump kujiuzulu


President Donald Trump speaks during a rally in Pensacola, Fla., Dec. 8, 2017.

Mseneta wanne wa Marekani Jumatatu walimtaka rais Donald Trump kujiuzulu kufuatia tuhuma za unyanyasaji wa kingono.

Wanawake watatu, ambao walikuwa wametoa tuhuma za kudhalilishwa mwaka jana, walirejelea matamshi hayo hiyo jana, na kusema kuwa ni wakati mwafaka kwa bunge kuanza uchunguzi kufuatia tuhuma nyingi zilizowalenga watu wanaoshikilia nyadhifa za juu, na ambao wamejiuzulu.

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha CNN, Seneta Mdemokrat Kirsten Gillibrand , anayewakilisha jimbo la New York, alisema ni sharti Trump ajiuzulu na kwamba shutuma zilizotolewa na wanawake waliosema aliwadhalilisha kingono, ni za kuaminika na za kuvungja moyo.

Aliongeza kwamba iwapo rais huyo hatajiuzulu mara moja, basi ni jukumu la bunge kuchukua hatua mwafaka na kuanza uchunguzi utakaolenga tabia zake.

Matamshi hayo ni sawa na ya Bernie Sanders, seneta huru anayewakilisha jimbo la Vermont, seneta mdemoktrat Jeff Merkeley kutoka Oregon na Cory Booker, seneta mdemokrat anayewakilisha jimbo la New Jersey, ambao walimtaka rais Trump kujiuzulu kufuatia hatua kama hiyo, iliyochukuliwa na seneta Al Franken wa Minnesota, baada ya tuhuma za udhalilishaji wa wanawake.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG