Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 21:40

Mary Robinson asisitiza amani ipatikane Congo


Mwakilishi wa UN kwa eneo la maziwa makuu Mary Robinson (R) na mwakilishi maalumu wa UN kwa Congo, Martin Kobler wakiwa Goma, Sept. 2, 2013.
Mwakilishi wa UN kwa eneo la maziwa makuu Mary Robinson (R) na mwakilishi maalumu wa UN kwa Congo, Martin Kobler wakiwa Goma, Sept. 2, 2013.
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa eneo la maziwa makuu barani Afrika, bi. Mary Robinson yupo Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kujionea hali halisi ya mapigano kati ya kundi la waasi wa M23 na serikali ya Congo na kuwashawishi waasi kuweka silaha chini ili kuweza kurejesha hali ya amani katika eneo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:05:23 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Sauti ya Amerika ilizungumza na kiongozi wa kundi la M23, Bitran Bisimwa na kutaka kwanza kujua wameipokea vipi taarifa hiyo na iwapo wapo tayari kurejea tena katika meza ya mazungumzo.

Wakati huohuo mazungumzo ya kitaifa yaliyopangwa kuitishwa Jumatano yameakhirishwa hadi Jumamosi.

Msemaji wa serikali ya Kongo Lambert Mende aliiambia VOA kwamba Kongo imesubiri kumuona bi. Mary Robinson kuonyesha msimamo wa dhati kuhusu amani mbele ya viongozi wa Rwanda kama jinsi anavyofanya kawa serikali ya Kongo.

“Tunachosubiri kutoka kwa jumuiya ya kimatafa na bibi Mary Robinson ni kuwa na hatua ya dhati kwa wenzetu wa Rwanda ili watekeleze majukumu yao yanayotokana na mkataba wa amani wa Addis Ababa. Kwa sababu tunachoshuhudia hivi sasa ni kwamba mwanachama mmoja wapo wa nchi za maziwa makuu wamekuwa wakikanyaga mkataba huo na kuendelea kuwaunga mkono wahalifu wa M23 ambao kwetu sisi ni magaidi kama magaidi wengine wa FDLR na kadhalika. Kwa bahati mabaya hadi sasa Rwanda inaendelea kufanya hivyo. Jumuiya ya kimataifa inatuomba kuzungumza na waasi wetu, lakini inapofika zamu ya Rwanda wamekaa kimya”.

Mary Robinson alisema kwamba harakati za kijeshi za UN za wiki iliyopita zilikuwa muhimu ili kuwahakikishia usalama wakaazi wa Goma. Kwenye ziara yake hii itakayo mpeleka pia Kampala na Kigali, Bi Robinson ameandamana na bwana Boubacar Diara mjumbe maalumu wa muungano wa Afrika, Russ Feingolg mjumbe wa Marekani kwa nchi za maziwa makuu na Koen Ferfaeke mjumbe wa muungano wa ulaya kwenye kanda ya maziwa makuu.
XS
SM
MD
LG