Wilaya ya Jing'an, katikati mwa Shanghai imeingia siku ya tatu ya shughuli zote kusitishwa kabisa isipokuwa usafirishaji wa bidhaa muhimu.
Shughuli ya upimaji ilifanyika mara tatu wakati shughuli za kawaida zimesitishwa, na watu kuruhusiwa kuondoka nyumbani wanapoenda kupimwa.
Maafisa wanaendelea kutoa chanjo dhidi ya Covid mjini humo wakilenga zaidi watu wazee.