Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 28, 2023 Local time: 08:24

Margaret Thatcher ameaga dunia


Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Margaret Thatcher (kati) akiwa pamoja na mashujaa wa vita vya Falkland katika maandamano Londo kuadhimisha miaka 25 ya vita vya Falkland Jun 17, 2007
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Margaret Thatcher afariki akiwa na umri wa miaka 87 kufuatia kupata kiharusi. Thatcher anasifiwa kwa kubadili muelekeo wa siasa za Uingereza wakati wa mihula yake mitatu madarakani.

Thatcher alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kushika madafraka ya juu ya Uingereza, aliyechukuliwa kuwa kiongozi mashuhuri anaeheshimiwa duniani mnamo miaka 11 ya uwongozi wake.

Katika kitabu juu ya wasifu wake Bi. Thatcher, aliyejulikana kama "Iron Lady" anasema mafaniko yake makubwa kama waziri mkuu ni kubadili sera ya Uingereza kutoka kile alichokieleza ujamaa usio na nguvu kuelekea jamii ya biashara huru.
XS
SM
MD
LG