Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 10, 2024 Local time: 21:13

Margaret Kenyatta atuzwa na Umoja wa Mataifa


Margaret Kenyatta (kushoto) mke wa rais wa Kenya
Margaret Kenyatta (kushoto) mke wa rais wa Kenya

Bi Kenyatta alitambuliwa kutokana na juhudi zake za kuokoa maisha ya kina mama na watoto wakati kina mama wanajifungua.

Umoja wa Mataifa leo Ijumaa umemtaja mke wa rais wa Kenya Bibi Margaret Kenyatta kuwa mtu maarufu kwa mwaka huu wa 2014, kutokana na kampeni yake ya kuokoa maisha ya mama na mtoto, maarufu kama “Beyond Zero.”

Bi Kenyatta alipokea tuzo yake hiyo katika ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko Gigiri, nje kidogo ya jiji kuu la Nairobi, wakati wa sherehe za kuadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa leo Ijumaa.

Akipokea tuzo hilo, Bi Margaret Kenyatta alieleza furaha yake kwa kutambuliwa na Umoja wa Mataifa, na kuongeza kuwa tuzo hilo ni la wote kina mama na baba wanaomuunga mkono katika juhudi zake za kufungua zahanati zenye vifaa vya kutosha, kusaidia kina mama wanapojifungua pamoja na wanao ili kuokoa maisha.

Takwimu za kisayansi zinaonyesha kuwa kina mama wengi wanaojifungulia watoto nyumbani wanapoteza maisha na watoto wengi wanaozaliwa katika hali hiyo hufa kabla ya kufikia umri wa miaka mitano.

XS
SM
MD
LG