Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 03:50

Marekani yasikitishwa na hatua ya ZEC kutangaza uchaguzi


Kiongozi wa upinzani Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad
Kiongozi wa upinzani Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad

Serikali ya Marekani imeelezea masikitiko yake kufuatia uamuzi wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza tarehe ya uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar.

Kauli iliyotolewa siku ya Ijumaa na Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema kwamba tume hiyo imechukua hatua hiyo bila kuwahusisha wadau wote kwenye mazungumzo ya kutatua mzozo wa kisiasa ulioikumba Zanzibar.

“Tunatoa wito kwa serikali ya Tanzania na Rais Magufuli kuhakikisha kumefanyika mazungumzo yanayohusisha pande zote ili kupata suluhisho la mzozo huo wa Zanzibar,” ilisema taarifa hiyo iliyotiwa saini na msemaji wa wizara hiyo, John Kirby.

Kirby ameongeza kwamba Marekani ingependa kuwa mwangalizi wa zoezi hilo la uchaguzi. Alitaka pande zote mbili ziimarishe amani na kuja pamoja kwa moyo wa kujitolea “kwa sababu Wazanzibari …na Watanzania wote wana haki ya kupata suluhisho kwa mzozo huo ambalo litatilia maanani matakwa ya wapiga kura na kuashiria kujitolea kwa serikali kuimarisha maadili ya kidemokrasia.”

XS
SM
MD
LG