Marekani imeweka vikwazo kwa vingozi wanne kutoka Burundi ikidai wamehusika kwenye mizozo inayoendelea nchini humo. Rais Obama amechukua hatua hiyo jumatatu kwa kutumia amri ya Rais. Wanne hao ni pamoja na waziri wa usalama wa umaa Alain Bunyoni, naibu mratibu wa idara ya polisi nchini, Godefroid Bizimana, aliekuwa mkuu wa ujasusi Godefroid Niyombare na aliekuwa waziri wa ulinzi Cyrille Ndayirukiye.
Marekani inalaumu Bunyoni na Bizimana kwa kudhulumu wapinzani wa rais Nkrunziza. Niyombare pamoja na Ndayirukiye wanalaumiwa kwa kujaribu kuipindua serikali ya rais Nkurunziza mwezi Mei. Amri hiyo ya Obama imefunga mali zote walizo nazo hapa Marekani pamoja na kuwazuia kusafiri hapa Marekani. Umoja wa Ulaya na umoja wa Afrika pia wamewawekea wanne hao vikwazo.