Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 27, 2022 Local time: 07:31

Marekani yaweka Russia kwenye orodha ya mataifa yanayofanya ulanguzi haramu wa binadamu


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken wakati wa kutolewa kwa ripoti ya ulanguzi wa binadamu.

Marekani Jumanne imeweka Russia kwenye orodha ya mataifa yenye sera au mtindo wa usafirishaji haramu wa binadamu pamoja na ajira za kulazimishwa, au ambayo vyombo vya usalama pamoja na makundi yanayoungwa mkono na serikali, yanajihusisha katika kutumia wapiganaji walio chini ya umri.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeweka orodha hiyo kwenye ripoti yake ya kila mwaka kuhusiana na ulanguzi wa binadamu chini ya idhini iliyobuniwa mwaka wa 2019 na bunge la Marekani, kwa jina State Sponsored Trafficking in Persons.

Russia imejitokeza mara kadhaa kwenye orodha hiyo kwa ajili ya uvamizi wake dhidi ya Ukraine mwezi Februari ,pamoja na kile ripoti hiyo imetaja kama kusababisha usafirishaji haramu wa mamilioni ya wakazi wa Ukraine wakiwa wakimbizi kwenye mataifa walikokimbilia.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken wakati wa kutoa ripoti hiyo amesema kwamba hali wanayopitia wakimbizi hao inafungua mlango kwa watu kuwatumia vibaya. Ubalozi wa Russia hapa Mjini Washington haujasema lolote kutokana na ripoti hiyo hata baada ya kuombwa na wanahabari kutoa tamko.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG