Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 13:02

Marekani yatwaa medali ya dhahabu kikapu Olimpiki


 Kevin Durant akisherekea kushinda medali ya dhahabu katika mpira wa kikapu katika michezo ya Rio kitu ambacho wamefanya tena huko Japan akiiongoza Marekani.
Kevin Durant akisherekea kushinda medali ya dhahabu katika mpira wa kikapu katika michezo ya Rio kitu ambacho wamefanya tena huko Japan akiiongoza Marekani.

Timu ya Marekani hatimaye imefanikiwa kuchukua medali ya dhahabu baada ya kuifunga Ufaransa kwa jumla ya pointi 87-82

Timu ya Marekani hatimaye imefanikiwa kuchukua medali ya dhahabu baada ya kuifunga Ufaransa kwa jumla ya pointi 87-82 katika fainali ya mpira wa kikapu siku ya Jumamosi huko Tokyo Japan.

Marekani ambayo ilianza kwa kupoteza mchezo wake wa kwanza katika Olimpiki dhidi ya Ufaransa ilikuwa imedhamiria kulipiza kisasi tangu kota ya kwanza ya mchezo huo.

Kevin Durant aliongoza Marekani kwa kufunga jumla ya pointi 29 na kuweka historia ya kuwa mtu wa tatu pamoja na Carmelo Anthony kuchukua medali za Olimpiki mara tatu.

Jayson Tatum alipachika jumla ya pointi 19, Damian Lillard na Jrue Holiday kila mmoja alifunga jumla ya pointi 11 kwa Amerika.

Na kwa upande wa Ufaransa ambayo ilitoa upinzani mkubwa kwa Marekani wachezaji waliyoipatia Ufaransa pointi katika mchezo huo ni Evan Fournier na Rudy Gobert kila mmoja alifunga pointi 16 na mchezaji Guerschon Yabusele alifunga pointi 13, Nando de Colo alikuwa na 12 na Timothe Luwawu-Cabarrot alifunga jumla ya pointi 11 kwa Ufaransa.

Ufaransa ilicheza fainali yake ya kwanza tangu mwaka 2000 kule Sydney Australia na kujipatia medali ya fedha.

Na katika pambano la pili kutafuta medali ya shaba Australia iliwashinda Slovenia kwa jumla ya pointi 107-93.

XS
SM
MD
LG