Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 03:31

Marekani yatuma wataalam Haiti


Rais wa Haiti aliyeuwawa Jovenel Moise kwenye picha ya awali. (wa pili kutoka kushoto)
Rais wa Haiti aliyeuwawa Jovenel Moise kwenye picha ya awali. (wa pili kutoka kushoto)

Marekani Jumapili imetuma timu ya kiufundi nchini Haiti kutathmini hali ya usalama na mahitaji mengine baada ya mauaji ya rais Jovenel Moise wiki iliyopita.

Haikuelezwa wazi ni taasisi zipi zimeshirikishwa, lakini timu hiyo inapanga kuwasilisha ripoti kwa rais Joe Biden itakaporudi nyumbani, kabla ya maamuzi kuchukuliwa juu ya kuhusika zaidi kwa Marekani katika mzozo mbaya unaokikumba kisiwa hicho cha Caribbean, afisa mwandamizi ameambia shirika la habari la Reuters.

Awali, Marekani ilitupilia mbali ombi la Haiti la kuitaka kusaidia kuzima ghasia zilizofuatia kuuwawa kwa rais Moise Jumatano. Kiongozi huyo aliuwawa kwa kupigwa risasi wakati akiwa nyumbani kwake, kwenye mji mkuu wa Port au Prince.

Idara ya polisi nchini humo imesema kuwa wamarekani wawili na wacolombia 26 baadhi yao wakiwa wanajeshi wa zamani, walihusika kwenye shambulizi hilo. Wengi wa washukiwa raia wa Colombia wangali wamfichoni wakati wakiendelea kusakwa .

Afisa mmoja kwenye utawala wa Biden amesema Marekani pia itashauriana na washirika wake wa kikanda pamoja na Umoja wa mataifa juu ya mzozo wa Haiti.

XS
SM
MD
LG