Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 29, 2020 Local time: 23:33

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetoa tahadhari ya kutosafiri Drc.


Rais joseph Kabila akikagua jeshi la Congo.

Wizara ya mambo ya nje ya marekani imetoa tahadhari ya kutosafiri katika jamhuri ya kidemkrasia ya Congo huku ikitoa amri ya maafisa wa serikali pamoja na familia zao walioko nchini humo kuondoka mara moja.

Onyo hilo limetolewa kutokana na uwezekano mkubwa wa kuzuka kwa ghasia kwenye maeneo mengi ya mji wa Kinshasa pamoja na miji mingine. Ghasia zimezuka nchini humo kutokana na swala la urais wa Joseph Kabila ambaye siku yake ya mwisho madarakani ni Decemba 19.

Kabila amekuwa madarakani kwa mihula miwili tangu mwaka wa 2001. Katiba ya nchi inamzuia kuwania muhula wa tatu lakini tume ya uchaguzi imesema kuwa haitaweza kuandaa uchaguzi hadi mwisho wa mwaka wa 2018 ingawa yeye mwenyewe hajatangaza hadharani nia yake ya kubaki madarakani.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG