Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 11:45

Marekani yatishia vikwazo zaidi kwa Russia


Victoria Nuland makamu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani anayehusika na mashauri ya Ulaya na Ulaya Mashariki.
Victoria Nuland makamu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani anayehusika na mashauri ya Ulaya na Ulaya Mashariki.

Afisa wa juu wa Marekani, anasema Washington, inatafakari kuweka vikwazo vipya kwa Russia, kama mpango wa kumaliza mapigano wa mwezi uliopita wa Minsk, hautaheshimiwa.

Pia imetuma ujumbe kwenda Ulaya, kuratibu makubaliano ya kumaliza mapigano na mataifa shirika.

Makamu wa wizara ya mambo ya nje kwa mashauri ya ulaya na ulaya mashariki Victoria Nuland, ameiambia kamati ya mashauri ya mambo ya nje katika baraza la uwakilishi.

Nuland amesema kwamba vikwazo vipya vinaweza kuwekwa kama Russia, itaendelea kuchochea mapigano mashariki mwa Ukraine, ama maeneo mengine ya nchi.

Kushindwa kutekelezwa kwa mpango uliowekwa saini nchini Belarus baina ya waasi wanaoungwa mkono na Russia na Ukraine kutasabisha vikwazo kuwekwa alisisitiza.

XS
SM
MD
LG