Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 14:13

Marekani yatishia kuiwekea vikwazo Uturuki


Rais Trump akiongea na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika Makao Makuu ya NATO, Brussels, Belgium Julai 11, 2018.
Rais Trump akiongea na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika Makao Makuu ya NATO, Brussels, Belgium Julai 11, 2018.

Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kuiwekea Uturuki vikwazo vikubwa iwapo haitamwachilia huru mhubiri raia wa Marekani ambaye amewekwa kizuizini nyumbani kwake nchini Uturuki.

Mgogoro huu wa kuzuiliwa raia wa Marekani umepelekea kuharibu uhusiano uliokuwepo kati ya washirika wa karibu wa muungano wa NATO.

Kulingana na shirika la habari la Reuters, utawala wa Trump umeongeza msukumo dhidi ya serikali ya Uturuki siku moja baada ya nchi hiyo kumweka Andrew Brunson, anayekabiliwa na mashtaka ya ugaidi na ujasusi, kizuizini nyumbani baada ya kuzuiliwa gerezani kwa muda wa miezi 21.

Kupitia ujumbe wa twitter, Rais Trump amesema kwamba Marekani itaiwekea Uturuki vikwazo vikubwa kwa kumzuilia mhubiri Brunson kwa muda mrefu, akimtaja Brunson kuwa mtu ambaye familia yake inamhitaji na ni mwenye maadili.

Trump amesema kwamba Uturuki imemsumbua sana mhubiri Brunson juu ya kuwa hajafanya kosa lolote na kutaka aachiliwe mara moja.

XS
SM
MD
LG