Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 02:59

Marekani yateuwa mjumbe mpya kwa Sudan


Mjumbe mpya wa Marekani kwa Sudan akiwa na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton
Mjumbe mpya wa Marekani kwa Sudan akiwa na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton

Uteuzi huu umetokea wakati hali ya wasiwasi ikidizi Abyei. Majeshi ya Kusini na Kaskazini mwa Sudan yameongezewa katika eneo hilo.

Utawala wa Obama Alhamis ulimteuwa Princeton Lyman kuwa mjumbe mpya maalum kwa Sudan. Tangazo la uteuzi wake lilitolewa huku hali ya wasiwasi ikizidi kuongezeka katika eneo la Abyei katikati mwa Sudan na kutishia mkataba wa amani wa Kaskazini na Kusini .

Lyman alikuwa amestaafu mwaka jana lakini akarejea kufanya kazi na utawala wa Obama kama mshauri wa maswala ya amani kati ya pande za Kusini na Kaskazini mwa Sudan. Sasa amepewa jukumu kubwa zaidi kama mjumbe maalum wa Marekani kwa Sudan wakati hali ikizidi kuwa tete katika eneo la Abyei.

Hali ya baadaye ya Abyei, eneo lenye utajiri wa mafuta lililoko katikati ya Sudan Kusini na Kaskazini bado haijaamuliwa, licha ya raia wa Sudan Kusini kupiga kura ya maoni na kuamua kujitenga na kuwa taifa huru.

Wakazi wa Abyei walitazamwia kupiga kura Januari mwaka huu kuamua ikiwa wanataka kujiunga na upande wa Kaskazini au wa Kusini, lakini kura hiyo iliahirishwa kufuatia mzozo juu ya nani wanastahiki kushiriki katika kura hiyo.

Taarifa za hivi karibuni zinasema wanajeshi wameongezwa katika eneo hilo la Abyei.

Lyman, zamani alihudumu kama naibu waziri katika wizara ya mambo ya nje ya Marekani, na anasifika kwa juhudi zake za kusaidia serikali ya Khartoum kurejesha majadiliano ya muda mrefu ya amani baina yakei na makundi ya waasi wa Darfur yaliyofanyika Doha nchini Qatar.

Lyman anachukua nafasi ya Jenerali mstaafu wa jeshi la angani la Marekani Scott Gration ambaye ameteuliwa na rais Barack Obama kuwa balozi ajaye wa Marekani nchini Kenya. Gration anasubiri kuidhinishwa na kamati ya baraza la Senate.

XS
SM
MD
LG