Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 22:35

Marekani yatathimini marufuku ya Taliban kwa wanawake


Marekani imekuwa ikitathmini athari za marufuku ya Taliban ya ajira kwa wanawake kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali huku ikitafakari  sera mbadala zinazoweza kuwekwa wazi hivi karibuni.

"Tumejitolea kuwatetea wanawake popote pale ambapo haki zao zinatishiwa, ikiwa ni pamoja na Afghanistan, kwani kwa bahati mbaya tunaendelea kuona hali ya kina na inazidi kuwa mbaya zaidi," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema Jumatano.

Hiyo ilikuwa wakati wa hotuba yake katika uzinduzi wa kwanza wa mkakati wa Marekani juu ya Usalama wa Kiuchumi wa Wanawake Duniani.

Maafisa wakuu wa Marekani wamerudia kuwasihi Taliban kubadili marufuku ya kuzuia wanawake kufanya kazi katika mashirika yasiyo ya kiserekali na kuhudhuria vyuo vikuu.

XS
SM
MD
LG