Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 28, 2020 Local time: 12:29

Marekani yataka maendeleo zaidi ya siasa Zimbabwe


Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe

Marekani inataka Zimbabwe ionyeshe maendeleo zaidi katika siasa nchini humo kabla ya vikwazo kuondolewa.

Marekani inasema Zimbabwe lazima ionyeshe maendeleo zaidi katika hali ya kisiasa kabla vikwazo dhidi ya Rais Robert Mugabe na washirika wake havijaondolewa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inasema wanadiplomasia wa Marekani waliwasilisha ujumbe huo wiki iliyopita kwa maafisa wa Zimbabwe katika mkutano uliofanywa na wajumbe wa serikali ya umoja ya Zimbabwe.

Taarifa iliyotolewa Washington Jumapili inasema Marekani ilitoa mfano wa kukamatwa kwa mwanaharakati mmoja mwanamke mjini Harare hivi karibuni na ghasia zilizovuruga mikutano ya mageuzi ya katiba wiki iliyopita. Taarifa hiyo inasema kadiri ambavyo ukiukaji wa haki za binadamu na vitisho dhidi ya wanaharakati wa siasa vinaendelea vikwazo vitaendelea dhidi ya Zimbabwe.

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG