Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 23:14

Marekani yatahadharisha raia wake kuwa makini na safari za nje


Saudi Arabia
Saudi Arabia

Wizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia mapema Jumatatu ilisema mtu mmoja alijitoa muhanga na kijilipua karibu na ubalozi wa Marekani katika mji wa magharibi wa Jeddah.

Wizara hiyo ilisema walinzi waliingiwa na mashaka kuhusu mtu mmoja na walipokuwa wakimfuata alijilipua. Mlipuko huo ulimuua mtu huyo na walinzi wawili walipelekwa hospitali kutokana na majeraha kidogo.

Ubalozi wa Marekani nchini Saudi Arabia uliripoti kwamba hakuna mfanyakazi wake aliyeuwawa wala kujeruhiwa. Imetoa tahadhari ya kusafiri Saudi Arabia na kuwataka raia wa Marekani kupunguza kusafiri hasa kwa safari zisizo na msingi.

XS
SM
MD
LG