Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 05, 2023 Local time: 19:15

Marekani yashindwa kupata Spika wa Bunge


Baraza la Wawakilishi la Marekani lilishindwa kumchagua Spika ajaye wa Bunge hilo Jumanne.

Kundi la wabunge waconservative wa Marekani waliendelea kumpinga mgombea wa chama cha Republikan Kevin McCarthy, kuongoza kikao cha 118 cha bunge.

Baada ya duru tatu za upigaji kura, Bunge liliahirisha mchakato huo hadi saa sita mchana Jumatano.

Ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 100 ambapo hakuna Mrepublikan au Mdemokrat aliyeshinda uspika wa Bunge katika duru ya kwanza ya upigaji kura kuwa kiongozi wa baraza lenye wajumbe 435.

McCarthy alishindwa uspika katika awamu tatu za upigaji kura, huku Warepublikan 20 wakimpinga katika duru ya mwisho.

Duru ya nne ya upigaji itafanyika leo, lakini haijulikani kama wapinzani wa McCarthy watamuunga mkono, au wagombea wapya wanaweza kuibuka.

XS
SM
MD
LG