Shambulio hilo liliua wanajeshi 13 wa Marekani na raia kadhaa, wakati Marekani ilipokuwa inaondoa wanajeshi wake nchini Afghanistan.
Shambulio hilo la bomu lilifanyika tarehe 26 Agosti mwaka wa 2021, wakati wanajeshi wa Marekani walikuwa wakijaribu kuwasaidia raia wa Marekani na Waafghanistan kutoroka katika kipindi cha machafuko kilichofuata baada ya Taliban kuchukua madaraka, na kuzidisha hisia kwamba Marekani ilishindwa baada ya miaka 20 ya vita.
“Alikuwa afisa mkuu wa ISIS-K aliyehusika moja kwa moja katika kupanga operesheni kwenye mlango wa Abbey kwenye uwanja wa ndege wa Kabul, na sasa hawezi tena kupanga njama au kufanya mashambilizi, ”msemaji wa masuala ya operesheni za kijeshi kwenye White House, John Kirby alisema katika taarifa.
Lakini hakutaja jina la afisa huyo.
Kundi la Afghanistan mshirika wa kundi la Islamic State, linalojulikana kama Islamic State Khorasan au ISIS-K, ni hasimu mkubwa wa Taliban.