Tathmini ya karibuni ya kila kipindi cha robo mwaka kuhusu madhara kwa raia iliyochapishwa na komandi ya Marekani ya Afrika, (AFRICOM), inathibitisha kwamba vikosi vya Marekani vilifanya mashambulizi ya anga karibu na mji wa Jilib, Februari 15, lakini inakanusha kwamba mashambulizi hayo yaliwauwa madaktari hao.
“Februari 17, 2024, komandi ilipokea ripoti moja ya chanzo cha habari cha mtandaoni ikisema kuwa raia wawili waliuawa kutokana na operesheni ya kijeshi ya Marekani katika eneo la Jilib, Somalia, Februari 15, 2024,” ripoti ya tathmini ya AFRICOM imeeleza.
“Komandi ilikamilisha uchunguzi wa taarifa zilizokuwepo na kuhitimisha kuwa mashambulizi ya anga ya Marekani, ya Februari 15, 2024, halikusababisha madhara kwa raia.”
Forum