Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 18:42

Marekani yasema yasikitishwa na kitendo cha Misri.


Wabunge wa Misri katika bunge lao la kwanza nchini Misri.
Wabunge wa Misri katika bunge lao la kwanza nchini Misri.

Mvutano waongezeka huko Misri huku Wamarekani wakiendelea kuzuiwa nchini Misri.

White house imesema imesikitishwa na kitendo cha Misri kuwazuia raia kadhaa wa Marekani kuondoka nchini humo.

Baadhi yao wameomba hifadhi kwenye ubalozi wa Marekani huko Cairo wakati mvutano ukiongezeka kuhusu uchunguzi wa serikali kuhusu makundi ya demokrasia yanayopewa fedha na nchi za nje.

Maafisa wa Marekani walisema jumatatu kuwa Washington imezungumza suala hilo na maafisa wa kijeshi wa Misri na kuweka bayana wasi wasi wao.

Msemaji wa White house Jay Carney amewaambia waandishi kuwa maafisa wanashughulikia kumaliza suala hilo haraka iwezekanavyo.

XS
SM
MD
LG