Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin wakati akizungumza na wanahabari kwa mara ya kwanza tangu alipolazwa hospitalini Januari mosi, kufuatia upasuaji wa kutibu saratani ya tezi dume, ametaja shambulizi hilo kuwa la kutisha, akiongeza kuwa visa kama hivyo havitavumiliwa na Marekani.
“Ni wakati wa kupunguza uwezo wao zaidi ya tulivyofanya awali,” Austin amesema Alhamisi, alipoulizwa ni kwa nini Marekani imechukua muda mrefu kujibu vikali zaidi ya mashambulizi 165 dhidi ya vikosi vya Marekani huko Mashariki ya Kati kufikia kati kati ya Oktoba mwaka jana.
Austin pia alionekana kupuzia taarifa iliyotolewa la Kataib Hezbollah ambalo ni kundi la wanamgambo linaloungwa mkono na Iran, kwamba linasitisha operesheni zake za kijeshi dhidi ya Marekani, akisema, “tunasikiliza kile watu wanasema, lakini tunatazama yale wanayafanya,” na kuongeza kwamba vitendo ndivyo muhimu Zaidi.
Forum