Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 18:26

Marekani yaonywa kuwa inaweza shindwa kulipa madeni yake


Ofisi ya bajeti katika bunge, Jumatano imesema wizara ya fedha ya Marekani itafikia miwsho wa uwezo wake wa kulipa madeni ya nchi kati ya Julai na Septemba.

Ili kuepekana na hali hiyo, labda kiwango cha kukopa cha dola trilioni 31.4 kiongezwe ama kusitishwa.

Katika ripoti iliyotolewa pamoja na mwelekeo wa bajeti ya mwaka, ofisi ya bajeti isiyo ya mrengo wowote kichama imeonya kufikia kiwango cha mwisho cha madeni kinaweza kufikiwa Julai.

Endapo mapato yanayotoka hazina mwezi Aprili yataendelea, kipindi ambacho Wamarekani wanajiandikisha kupata fedha zao walizolipia kodi hali hiyo inaweza kujitokeza.

Kiwango cha fedha zinazo ingia hazina na namna hali ya uchumi wa Marekani ulivyo katika miezi ijayo, kunafanya kuwa ngumu kwa maafisa wa serekali kubashiri lini hasa hazina inaweza kuanza kushughulikia malipo ya baadhi ya shughuli zilizo chini yake.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG