Mashindano ya Olimpiki Jumanne yaliingia katika siku yake ya nne mjini Rio De Jenairo, Brazil. Kufikia Jumatatu usiku, Marekani ilikuwa ikiongoza kwa wingi wa medali, huku ikiwa na medali tano za dhahabu, saba za fedha na saba za shaba.
China ilikuwa kwenye nafasi ya pili ikiwa na medali tano za dhahabu, tatu za fedha na tano za shaba. Japan, Russia na Italia zilikuwa zinafuatana kwa wingi wa medali.
Baadhi ya nyota walioshinda dhahabu hiyo jana, ni pamoja na muogeleaji maarufu wa Marekani Michel Pheps ambaye kufikia sasa ameshashinda medali 23 katika mashindano yote ya Olimpiki aloshiriki, na hivyo basi kuwa mwanariadha aliyepata medali nyingi Zaidi za dhahabu katika historia ya mashindano ya msimu wa kiangazi ya Olimpiki.