Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 13, 2025 Local time: 12:34

Marekani yamwekea vikwazo mwanasheria mkuu Zimbabwe


Mshirika wa Rais Mugabe awekewa vikwazo.
Mshirika wa Rais Mugabe awekewa vikwazo.

Marekani imemwekea vikwazo mwanasheria mkuu wa Zimbabwe na kusema vitendo vyake vinadharau taasisi za kidemokrasia nchini humo.

Wizara ya fedha Marekani leo imemshutumu Johannes Tomana mshirika wa rais Robert Mugabe kwa kuwalenga wapinzani fulani kwa ajili ya kuwatesa. Imesema hatua zake zinatishia utawala wa sheria nchini Zimbabwe na kuleta utete kwenye serikali yao ya ushirikiano.

Vikwazo hivyo vina maana raia wa Marekani hawaruhusiwi kufanya biashara na Tomana na kwamba mali zake zilizoko Marekani zinazuiwa.

XS
SM
MD
LG