Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 13:39

Marekani yamtaka Gadhafi aondoke.


Baadhi ya wafuasi wa Gadhafi wakiwa wamebeba picha zake.
Baadhi ya wafuasi wa Gadhafi wakiwa wamebeba picha zake.

"Njia moja tu ya kusonga mbele ni kwa Bw. Gadhafi kuachia madaraka" alisema afisa wa Marekani.

Maafisa wa Libya na Marekani wanasema wawakilishi kutoka serikali hizo mbili walifanya mazungumzo ya moja kwa moja hivi karibuni lakini Washington ilisisitiza kuwa lengo kuu lilikuwa ni kuwasilisha ujumbe wa wazi na thabiti kwamba kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi lazima aachie madaraka.

Afisa wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani amesema mkutano huo wa mara moja haukuwa wa makubaliano na kwamba njia moja tu ya kusonga mbele ni kwa Bw. Gadhafi kuachia madaraka.

Alisema mazungumzo hayo yalifanyika Jumamosi na kumhusisha waziri mdogo wa mambo ya nje Jeffrey Feltman, afisa wa juu wa mambo ya nje anayeshughulikia sera za mashariki ya kati. Wajumbe wanne wa karibu wa Bw.Gadhafi.

Awali msemaji wa serikali ya Libya Moussa Ibrahim alielezea mazungumzo hayo ambayo yalifanyika Tunisia kama hatua ya kwanza ya mazungumzo . Alisema serikali ya Libya haitaki kukwama katika masuala ya siku za nyuma na wangependa mazungumzo zaidi.

XS
SM
MD
LG