Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 10:39

Marekani yalaani mauaji ya raia 13 Uturuki


Ned Price (Nicholas Kamm/Pool via AP)

Marekani imelaani mauaji ya raia 13 wa Uturuki yaliyo fanywa na wanamgambo wa Kikurdi kaskazini mwa Iraq.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Ned Price alisema katika taarifa yake Jumapili jioni kuwa : "Tunasimama pamoja na washirika wetu wa NATO Uturuki na tunatoa pole kwa familia za waliouawa katika mapigano ya hivi karibuni."

Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar alisema mapema Jumapili kwamba waathirika walitekwa nyara na kuuawa na wanachama wa Chama cha Wafanyakazi cha Kurdistan, au PKK.

Hulusi Akar
Hulusi Akar

Akar alisema miili hiyo iligunduliwa katika mkoa wa Gara, karibu na mpaka wa Uturuki na Iraq, wakati wa operesheni dhidi ya PKK ambapo vikosi vya Uturuki viliwauwa wanamgambo 48.

Taarifa katika tovuti ya PKK ilisema inashikilia wafungwa wa vita, pamoja na majasusi wa Uturuki, polisi na wanajeshi, na kwamba waliuawa kutokana na mapigano.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG