Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 16:49

Marekani yajiandaa kulinda maslahi yake Iraq


Meli ya Marekani USS George H.W. Bush.
Meli ya Marekani USS George H.W. Bush.
Marekani imeagiza kupelekwa kwa meli inayobeba ndege za kivita na silaha katika ghuba ya uajemi, tayari kujibu mgogoro unaoendelea nchini Iraq.

Msemaji wa Pentagon John Kirby amesema waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel alitoa amri hiyo Jumamosi kwa meli hiyo kwa jina USS George H.W. Bush kupelekwa kwenye ghuba ya uajemi kaskazini.

Kirby anasema hatua hiyo ni muhimu na kwamba inawapa uwezo wana jeshi wa Marekani uwezo wa kuchukua hatua ikibidi kulinda maisha ya wamarekani na maslahi yake nchini Iraq.

Wanamgambo wa kundi la Islamic State of Iraq and Levant katika siku za karibuni wamedhibiti maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo na wanaendelea kusogea kuelekea mji mkuu Baghdad.
XS
SM
MD
LG